GET /api/v0.1/hansard/entries/1096614/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1096614,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1096614/?format=api",
"text_counter": 127,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mvita, ODM",
"speaker_title": "Hon. Abdullswamad Nassir",
"speaker": {
"id": 2433,
"legal_name": "Abdulswamad Sheriff Nassir",
"slug": "abdulswamad-sheriff-nassir"
},
"content": "Katika mwezi wa Novemba 2019, lile Shirika la KPA lilipeana shilingi bilioni 18.7 kwa Serikali kama faida na kulipa ushuru wa shilingi billioni 6. Hizo ni pesa ambazo haziwezi kuundwa ikiwa sio wale watu. Sasa hivi, tukichelewa sana, nasikia wanajaribu kukata mambo ya bonus na overtime . Naomba Kamati ya Leba, kama ile ya Uchukuzi iliyokwenda Mombasa na kukaa na wachuuzi wa Mama Ngina na Public Beach, walichukulie swala hili kwa haraka inavyowezekana. Hawa wafanyikazi wakivunjika moyo, itakayopoteza ni nchi nzima, sio Mombasa peke yake. Tunakubali kuwa watu wa Mombasa ndio watakaoumia, lakini nawakumbusha kuwa kidole kikiumia, ni mwili mzima utakaoumia. Asante."
}