GET /api/v0.1/hansard/entries/1096616/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1096616,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1096616/?format=api",
"text_counter": 129,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mwea, JP",
"speaker_title": "Hon. Josphat Kabinga",
"speaker": {
"id": 13441,
"legal_name": "Josphat Kabinga Wachira",
"slug": "josphat-kabinga-wachira-2"
},
"content": " Asante sana, Mhe. Spika. Hata mimi nainuka kusema kuwa tumechukulia swala hilo kwa uzito sana. Tumekuwa tukifuatilia na Wizara ya Fedha. Kila wiki, tunaahidiwa ya kwamba tutapata jawabu lakini hatujalipata. Ningetaka usaidizi wako kwa sababu naelewa kuwa kazi ya Kenya Ports Authority iliwekwa katika Wizara ya Fedha hivi juzi. Kwa hivyo, labda wako na changamoto ya kutupa jawabu lakini hiyo si sababu ya kutolileta. Namuelewa sana Mheshimiwa na uzito alio nao kutoka kwa wafanyikazi wa Bandari. Kwa hivyo, ningetaka usaidizi wako ili Wizara husika iamrishwe na Bunge kuja mbele ya Kamati kwa lazima. Sisi pia hatungetaka wafanyikazi wafe moyo na bado tuko na tunataka kuwafanyia kazi katika Bunge. Kwa hivyo, tuko tayari kama Kamati ya Leba na Social Welfare . Ni Wizara husika ambayo inatulet down. Asante."
}