GET /api/v0.1/hansard/entries/1097109/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1097109,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1097109/?format=api",
"text_counter": 622,
"type": "speech",
"speaker_name": "Jomvu, ODM",
"speaker_title": "Hon. Bady Twalib",
"speaker": {
"id": 1612,
"legal_name": "Bady Twalib Bady",
"slug": "bady-twalib-bady"
},
"content": "Tukiangalia tarakimu, takribani asilimia 80 ya nchi hii ni sehemu kame. Vile vile, tunategemea asilimia 20 peke yake ili kuweza kukimu mahitaji ya lishe katika nchi hii. Kwa wakati huu mgumu, lishe ni lazima kwa kila mwananchi ndiyo asipate shida ya kukosa chakula. Hali hii haiwezekani katika nchi hii ikiwa sehemu kubwa ni kame. Ndiyo tunaona Serikali inajizatiti kwa wakati huu tukiangalia projects kama Galana Kulalu kule Tana River, ili kuweza kuinua wananchi wake waweze kupata chakula. Kitu kidogo ambacho mimi nitaweza kusema ni kulikuwa na kiongozi marehemu ambaye aliitwa Thomas Sankara. Aliwaambia watu wake kwamba yule ambaye anakupatia chakula kwa mdomo basi ataweza kukutawala ama kuwa colonise . Hivyo basi, akawahimiza wananchi wake lazima wafanye mambo ya kilimo ili kuweza kujilisha katika nchi ile. Ilioneka maajabu kwa sababu nchi ile iliweza kubadilika na mengi hivi sasa yanachukuliwa kama mfano mkubwa sana wa wakati ule."
}