GET /api/v0.1/hansard/entries/1097111/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1097111,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1097111/?format=api",
    "text_counter": 624,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Jomvu, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Bady Twalib",
    "speaker": {
        "id": 1612,
        "legal_name": "Bady Twalib Bady",
        "slug": "bady-twalib-bady"
    },
    "content": "Tukiangalia wakati huu wa korona, unyunyizaji maji kwa mashamba tunaosema, watu wakipata maji wanaweza kufanya ukulima katika sehemu wanazoiishi. Tumeona hivyo katika sehemu za Nairobi na zingine. Lakini nikisema kuwa ni haki ya kimsingi kila mmoja kupata maji, leo nashangaa kwa sababu kuna sehemu tangu tupate Uhuru mpaka leo, bado tunalia kuna shida ya maji. Mfano ambao nitatoa katika jambo hili ni sehemu yangu pale Jomvu. Wiki iliyopita kulikuwa na maadamano makubwa sana katika sehemu inayoitwa Bangladesh. Vile vile, watu hawana raha katika sehemu inayoitwa Ganahola. Mpaka leo tangu tupate Uhuru, wananchi hawa wanapata maji kupitia kwa mfadhili ambaye ni Mombasa Cement. Hili ni jambo ambalo haliwezekani na ni lazima kama Serikali tusimame kidete kuhakikisha kwamba haki hii ya kimsingi kwa kila mwananchi ipatikane."
}