GET /api/v0.1/hansard/entries/1097114/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1097114,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1097114/?format=api",
"text_counter": 627,
"type": "speech",
"speaker_name": "Jomvu, ODM",
"speaker_title": "Hon. Bady Twalib",
"speaker": {
"id": 1612,
"legal_name": "Bady Twalib Bady",
"slug": "bady-twalib-bady"
},
"content": "Kimunya. Ni kweli kabisa leo ukienda Dubai, ilikuwa nchi kame. Lakini jangwani kumekuwa na maajabu. Leo kule Dubai kuna soko kubwa sana la matunda ambalo nina hakika pengine unalijua Mhe. Naibu Spika wa Muda. Hii ni kwa sababu ni soko maarufu na lina supply matunda katika kila sehemu. Dubai hivi sasa wanataka kukuza mchele ambao watatumia na vile vile kufanyia biashara. Hivi sasa ukifika huko, unatumia maji na ni jangwani na hii ni mfano wa kuigwa. Lakini jambo nzuri ambalo ningependa kusema ni kwamba si bora kama viongozi katika nchi hii kutoa mifano ya Dubai na kwingineko. Inatakikana kama Kenya tuwe mfano wa watu wa sehemu zingine. Wakituona wanasema: “Angalia vile Kenya imeweza kuwa!”"
}