GET /api/v0.1/hansard/entries/1097115/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1097115,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1097115/?format=api",
    "text_counter": 628,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Jomvu, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Bady Twalib",
    "speaker": {
        "id": 1612,
        "legal_name": "Bady Twalib Bady",
        "slug": "bady-twalib-bady"
    },
    "content": "Katika Mswada huu naangalia kama bodi hii itaweza kudhibiti na kusimamia maswala haya ili asilimia 80 ambayo ni sehemu kame iweza kuipunguza. Na kama nchi itaweza kulishwa na asilimia 20 iweze kupanua sehemu hizi ziweze kuzalisha, basi hatutakuwa na shida. Leo mimi nataka kutoa mfano mzuri sana wa hapa Uganda. Wana shida za mambo mengine lakini si chakula. Wanatoa chakula mpaka hivi sasa hawajui chakula kile watakipeleka wapi. Kwa hivyo tusitoe mifano ya mbali. Mifano ya hapa karibu ndiyo ya kuigwa. Tukitumia mifano hiyo, sisi tunaweza kuupitisha Mswada huu. Mhe. Sankok amesema kuwa leo ameishi katika ndoto. Kwamba alipokuwa katika chuo kikuu, aliona jambo kama hili litakuja kutokea. Leo hii amekaa hapa akiwa kiongozi kuona kuwa jambo lile alilolishauri wakati ule kama lingefanyika kwa pesa kidogo, leo katika kulifanya, litagharimu pesa nyingi. Si kuwa nchi haina pesa. Kuna miradi mikubwa ambayo inafanyika, kwa mfano, Expressway. Tunaona kilomita 21 ya barabara nzuri inaweza kubadilisha The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}