GET /api/v0.1/hansard/entries/1097116/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1097116,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1097116/?format=api",
    "text_counter": 629,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Jomvu, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Bady Twalib",
    "speaker": {
        "id": 1612,
        "legal_name": "Bady Twalib Bady",
        "slug": "bady-twalib-bady"
    },
    "content": "asilimia kubwa ya nchi ambayo ni kame na ikawa inaweza kuzalisha chakula. Mambo haya ni ya kimsingi. Nimepeana tu mfano mmoja. Hii ni mara yangu ya pili kuhudumu katika Bunge hili. Mhe. Naibu Spika wa Muda, mara yangu ya kwanza ilikuwa mwaka wa 2013, tukiwa pamoja na wewe humu Bungeni. Tulifanya tena kampeni mwaka wa 2017 tukawa na haki ya kimsingi katika maeneo yetu. Nakumbuka siku moja nikifanya kampeni nilisema nitajenga shule katika sehemu fulani ambayo haikuwahi kuwa na shule tangu uhuru. Aliinuka kijana mmoja akaniambia: “Beba shule yako uende nayo kwa sababu hatuna chakula hapa.” Kwa hivyo, masuala ya chakula ni muhimu kila mahali. Ikiwa hatutaweza kuwapatia watu wetu lishe bora, basi watu hawa watageuka kuwa watumwa wa watu wengine ambao tutakuwa tukiwapatia chakula cha misaada. Kenya yetu haiwezi kuwa na watumwa ndani yake. Tuna uwezo wa kuwapatia watu wetu chakula bora ili wakaishi maisha bora."
}