GET /api/v0.1/hansard/entries/1097656/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1097656,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1097656/?format=api",
    "text_counter": 135,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Bahati, JP",
    "speaker_title": "Hon. Kimani Ngunjiri",
    "speaker": {
        "id": 1179,
        "legal_name": "Onesmas Kimani Ngunjiri",
        "slug": "onesmas-kimani-ngunjiri"
    },
    "content": " Thank you, Hon. Speaker, for giving me this opportunity. Ningetaka kuangazia mambo mawili au matatu. Ya kwanza, nashukuru Mhe. Duale kwa kuleta jambo nyeti ambalo tunafaa kuangalia kwa urefu. Kwa sababu ya ujuzi wake, tunamheshimu. Ni mtu anajua mambo mengi. Ametuongoza kwa hili Bunge. Lakini ningekuwa na maoni ya kufikiria. Hii mambo ya BBI iko kortini na inaenda Korti ya Upeo. Tuwape nafasi kwa kisheria waendelee na mambo yao. Lakini sisi kama Bunge, kuna mambo matatu nyeti tunafaa kuangalia. Moja, kuna shida kubwa kwa sababu ya ugonjwa wa COVID-19. Hilo ni jambo muhimu ambalo tunafaa kulifikiria katika Bunge. Katiba mpya tunaletea nani wakati watu wanakufa? Ukifanya uchunguzi wako katika vyumba vya kuhifadhi maiti, utashangaa! Wacha wale wanatangazwa! Watu wetu wameisha kwa sababu ya ugonjwa wa COVID-19. Tunangoja pesa za kununua dawa. Kama tunaendesha haya mambo ya BBI, ile pesa iliyotumika ingesaidia sana watu wetu wasikufe. Tungekuwa na watu ambao tunajadiliana vile watapiga kura kwa sababu wangekuweko. Hawangekuwa wamekufa! Tunatengeneza mambo gani ilhali watu wetu wameisha? Sisi tumechaguliwa na wananchi na itaonekana vibaya kama hatutetei mambo nyeti yanayohusu watu wetu. Ukiangalia shida iko mbele yetu, ile muhimu ni ng’ombe za wafugaji zimekwisha. Tunahitaji kujadiliana watafanyiwa nini kwa sababu ya ng’ombe wao. Hilo ni jambo muhimu kwa sababu ni uchumi ambayo tumetengeneza tayari. Huo uchumi unaisha. Kama hatuna nafasi ya kuichunga, tutafanya namna gani? Jambo lingine ni kuwa ni muhimu sana tujue tutachunga watu wetu namna gani. Tutawaangalia namna gani kama tunafikiria uchaguzi wa 2022 ufanywe kwa njia nzuri? Jambo la umuhimu ni tupitishe haya majina tumeletewa ili kuhakikisha Chebukati ako na watu wa kutosha asikosolewe na korti. Tunafaa kutengeneza mikakati mizuri ya uchaguzi wa 2022. Tunaendesha Hoja ya BBI na tutasahau tunaelekea uchaguzi. Mikakati ambayo tunataka kuweka ili uchaguzi uwe wa wazi itakuwa shida. Itafika pahali Chebukati atasema: “Mlinipa pesa kuchelewa na kwa hivyo, sikuweza kuleta vifaa vinavyotakikana.” Saa hii kunatakikana usajili wa wapiga kura. Anafaa awe na pesa. Jambo hili ndilo tulikuwa tunazungumzia kuona vile tutasaidia ili uchaguzi wa 2022 uwe ni uchaguzi wa kubalika na pande zote. Ni muhimu sana, The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}