GET /api/v0.1/hansard/entries/1097756/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1097756,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1097756/?format=api",
"text_counter": 60,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kilifi CWR, ODM",
"speaker_title": "Hon. (Ms.) Gertrude Mwanyanje",
"speaker": {
"id": 13245,
"legal_name": "Gertrude Mbeyu Mwanyanje",
"slug": "gertrude-mbeyu-mwanyanje"
},
"content": " Asante, Mheshimiwa Spika. Nasimama kuunga mkono Hoja hii ya kuchaguliwa kwa makamishna wa TSC. Nataka kuunga mkono kuchaguliwa kwa kina mama kama makamishna ili kuongezea ile idadi ambayo ipo kwa TSC. Mhe. Spika, nataka tu kuzungumzia kamishna Madam Christine Kahindi ambaye anatoka Kilifi. Amekuwa mwalimu kwa miaka nyingi. Ameweza kuweka nidhamu kwa zile shule ambazo amefundisha na kuelekeza watoto. Ni mwalimu ambaye amekuwa wa hali ya juu na alikuwa mwalimu bora zaidi katika jimbo la Kilifi mwaka wa 2017. Isitoshe, katika zile shule ambazo amefundisha kama Jaribuni Secondary, Kilifi Township, Majaoni Secondary na Katana Ngala Girls, amekuwa mwalimu wa kike ambaye ameleta nidhamu. Hakuna wakati hata mmoja katika shule zake ambapo wanafunzi waligoma au kuchoma shule. Kwa hivyo, ni mwalimu mwenye taadhima na kwa sababu ya hilo, mimi naunga mkono kupandishwa cheo kwake. Akiwa mwalimu pale Majaoni na katika hali ya ugumu ya masomo Kilifi Kaunti, aliweza kutoa 'A'. Kwa hivyo, mimi naunga mkono. Asante Mheshimiwa Spika. Sisi Wanakilifi tunafurahia kupandishwa cheo kwa mwalimu huyu. Tunamuenzi sana. Asante, Rais Uhuru Kenyatta. Asante sana."
}