GET /api/v0.1/hansard/entries/1097825/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1097825,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1097825/?format=api",
"text_counter": 129,
"type": "speech",
"speaker_name": "Likoni, ODM",
"speaker_title": "Hon. (Ms.) Mishi Mboko",
"speaker": {
"id": 874,
"legal_name": "Mishi Juma Khamisi",
"slug": "mishi-juma-khamisi"
},
"content": " Asante sana, Mheshimiwa Spika kwa kunipa nafasi na mimi niweze kuunga mkono Hoja hii maalum ambayo imetuleta leo kuzungumzia wateuliwa wanne katika Tume ya Uchaguzi na Mipaka. Naunga mkono kwa sababu wateuliwa hawa wamefuzu katika tajriba ya kielimu, uzoefu wa kikazi katika utawala wa umma, usimamizi wa sekta za umma na mambo ya kisheria. Pia wateuliwa hawa hawakuwa na dosari katika mambo yoyote ya uhalifu ama kuwa na hoja ambayo ingebadilisha maadili yao ya kibinafsi. Tumeona ya kwamba Mheshimiwa Uhuru amezingatia jinsia; Ameweka kina baba wawili na kina mama wawili. Hivyo ni kutuonyesha ya kwamba kule tunakoelekea tutaweza kupata asilimia hamsini kwa hamsini katika uwakilishaji katika sekta zetu za kitaifa ama sekta zetu za umma. Kwa muda mrefu, tumekuwa tukisema ya kwamba tume hii ya Uchaguzi na Mipaka imekosa akidi. Akidi ni quorum. Imekuwa haina kiasi cha makamishna ambao wanaweza kufanya kazi za Tume hii. Tutakapomaliza zoezi hili, tutaweza kuwa na akidi inayofaa kuendeleza kazi za uchaguzi na zile za mipaka. Mheshimiwa Spika, katika wateuliwa hawa, kuna mama mmoja anaitwa Juliana Cherere. Mama huyu nilimjua kwa muda mrefu sana akiwa mwalimu katika kaunti yangu ya Mombasa. Ameweza kusomesha katika shule kadhaa na pia amefanya kazi katika sekta za umma katika mambo ya utawala wa umma na pia usimamizi. Ameonyesha tajriba ya hali ya juu sana katika kazi The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}