GET /api/v0.1/hansard/entries/1097831/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1097831,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1097831/?format=api",
"text_counter": 135,
"type": "speech",
"speaker_name": "Likoni, ODM",
"speaker_title": "Hon. (Ms.) Mishi Mboko",
"speaker": {
"id": 874,
"legal_name": "Mishi Juma Khamisi",
"slug": "mishi-juma-khamisi"
},
"content": " Asante sana, Mheshimiwa Spika. Nataka nikubali ya kwamba ni wakati mwafaka kuweka sura ya Kenya katika uteuzi wetu. Isitoshe, tunaposema tunataka kuweka sura ya Kenya, lazima tuzingatie ya kwamba kwa kihistoria kuna jamii au makabila ambayo yalikuwa yamesahaulika pahali pakubwa sana katika uteuzi. Hivyo basi, wakati Rais wetu anafanya uteuzi, ni muhimu afikirie na kuwapa nafasi nyingi sana makabila yaliyokuwa yametengwa na yale ambayo ni machache. Hii ni kwa sababu hivi leo ukifika Pwani, kuna makabila ambayo yametengwa; Digo, Duruma, Pokomo, na Bajuni. Wako Pwani lakini wametengwa zaidi hata kule Pwani. Hata tukija huku Bara, sehemu ambayo Mheshimiwa Spika wetu ametoka kule Mbeere imetengwa zaidi. Kabila la Mbeere ni kabila ambalo katika ile hali ya kule kwao ni kuwa wametengwa zaidi. Wametengwa na wamewekwa kama kundi la wachache zaidi. Kwa hiyvo, ni wakati mwafaka hawa ndio wawe wakifikiriwa ili waweze kufikia yale makabila makubwa ambayo yamekuwa na nafasi kubwa katika katika Taifa letu la Kenya, ili kila mmoja aweze kuwa yeye pia aweza kupata ile keki ya taifa kwa njia ya usawa. Tume hii ni muhimu sana na tunaamini hawa walioteuliwa wataweza kuonyesha maadili mema ambayo yataleta dhamani zaidi katika mambo ya uchaguzi na mipaka. Maadili ambayo yataweza kuzuia ghasia na michafuko ya kisiasa haswa wakati wa upigaji kura au wakati watu wanavyojiandikisha mambo ya kura. Kwa hivyo, akina mama wenzetu mulioteuliwa pale, tunajua mama ni kiungo muhimu katika mambo ya Amani. Mama ni kiungo muhimu katika mambo ya kuunganisha. Mkiweza kuingia katika Tume ile mutafute njia ya kuondoa changamoto zilizoko sasa na kuweza kuleta atatuzi na kwamba kuwe na historia ya kwamba ifikapo mwaka 2022 tutakuwa na uchaguzi ulioshwari, wa amani na wa haki ili Kenya iweze kusonga mbele kama taifa letu. Ninashukuru sana hawa wote waliochaguliwa kwa sababu wote wanatajiriba na wanauwezo. Wameweza kuwa na uzoevu na mambo haya yote ambayo yataweza kuwe kwenye Tume. Kwa sababu ya wakati sitazungumza zaidi, nataka nishukuru na niunge mkono. Asante sana, Mhe. Spika"
}