GET /api/v0.1/hansard/entries/1098132/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1098132,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1098132/?format=api",
    "text_counter": 289,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Asante, Bi. Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii kuchangia Mswada wa elimu ya mafunzo ya kiufundi. Kwanza, ninampongeza Sen. (Dr.) Milgo na Kamati ya Elimu ya Bunge la Seneti, kwa Mswada huu ambao utasaidia vijana pakubwa humu nchini. Pia Mswada huu utasaidia wale waliyohitimu katika masomo mbalimbali lakini hawana elimu ya kiufundi. Ufundi kama useremala, uashi au ujenzi na kadhalika, unahitajika ili kusaidia taifa hili kusonga mbele katika kuendelea duniani. Masomo ya kiufundi yalianza zamani lakini kwa kuwa hakuna mfumo wa kuyabeba, imekuwa ikifanyika kibahati nasibu. Kwa mfano, nilipoingia kidato cha kwanza miaka mingi iliyopita, nilifanya somo la useremala na ufundi wa kujenga majiko na vyombo vingine. Kwa hivyo, sio jambo la ajabu kufanya masomo ya kiufundi. Ni jambo ambalo limekuwa. Hata mimi baadaye, ufundi huo ulinisaidia kufanya kazi ndogondogo nyumbani kwangu. Masomo ya kiufundi ni muhimu sana katika Jamhuri na yatasaidia vijana ambao hawakubahatika kupata masomo ya chuo kikuu. Haimaanishi kuwa waliosoma hadi chuo"
}