GET /api/v0.1/hansard/entries/1098139/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1098139,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1098139/?format=api",
    "text_counter": 296,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Haya ni mafunzo yanayotolewa katika kituo cha elimu ya kiufundi. Hata hivyo,, haitoi mwongoza na kupeana mfano wa masomo ya kiufundi kama vile useremala. Hata hivyo, elimu ya kiufundi haitoi mwongozo. Mfano wa masomo ya kiufundi ni useremala, masomo ya ufundi wa kujenga, masomo ya kiufundi ya kuunganisha umeme. Tuna masomo mengine ya kiufundi kama ya kupika, kutengeneza vikapu na kadhalika. Kuna haja ya kuangalia kwa undani haya masuala ya vipi tutaweza kutambua masomo ya kiufundi. Haya maelezo yalipeanwa sasa kwa Mswada huu hayatoi mwongozo kamili wa masomo ya kiufundi. Jambo la kufurahisha ni kwamba serikali zetu za kaunti zinapewa jukumu katika masomo haya ya kiufundi. Tumeona kwamba wengi wanapigania kazi za kuajiriwa lakini kazi nyingi siku hizi ni za kujiajiri mwenyewe na masomo ya kiufundi kama haya yanatoa fursa ya kuweza kujiajiri mwenyewe. Tatu, kuweka msingi ama standards ya kuweza kutambua wale wanaofanya masomo ya kiufundi pia imekuwa swala nzuri sana kwa sababu tuanona wengi waliofanya kazi za ufundi hawana cheti isipokuwa wale wanaoenda kupitia kwa serikali ambao wengi wanashindwa kufanya hivyo kwa sababu wanatakikana waende wakaandike mtihani wa masomo ya theory lakini hawakufaulu kiingereza. Kwa hivyo, inakuwa shida wao kuweza kupata shahada kupitia mfumo wa kisasa. Mswada huu utatoa fursa kwa wale ambao wamefanya ile kazi ambayo wanatakikana kufanya, kwa mfano, kujenga, useremala na fundi wa mifereji. Wataweza kufanya mitihani kama ile bila ya kuwa na hofu kwamba wataanguka kwa sababu ya kutosoma somo la kiingereza kwa mitihani mingi huandikwa lugha ya Kiingereza. Hivi vyuo pia vitakuwa na mfumo kamili ambo unatambulika ili ukiwa unatoka kaunti moja kwenda kaunti nyingine unaweza kujiunga na chuo katika sehemu nyingine na uendelee na masomo yako bila ya kuwa na matatizo yoyote."
}