GET /api/v0.1/hansard/entries/1098143/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1098143,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1098143/?format=api",
"text_counter": 300,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "tuondoe tuweke mfumo wa kuwa na board of management ili kila anayekuwa pale anakuwa ni msimamizi vyuo vile ili tuweze kuhakikisha kwamba tuna usimamizi sawa sawa. Tumeona kwamba zamani kule Mombasa tulikuwa na chuo cha Mombasa Islamic Institute ambacho kilikuwa kinatoa mafunzo kama haya. Baadaye kililegeuzwa kikawa polytechnic na kikaendelea kuwa polytechnic mpaka mwaka juzi katika mwaka wa 2002 wakati kilipofanywa kuwa chuo kikuu. Hiyo imepoteza nafasi kubwa kwa watu wa Mombasa kwa sababu yale masomo ya kiufundi ambayo yalikuwa yanafanyika pale, hivi sasa hayapatikani na hii inafanya watu wengi waweze kuondoka kuja kutafuta masomo yale katika sehemu zingine katika nchi. Kwa hivyo, hizi vyuo vya kiufundi ambazo tunazungumzia hapa zitasaidia pakubwa kuleta elimu ya kiufundi mashinani kwa sababu elimu hii itasaidia zaidi wale ambao wanapatikana mashinani na itaweza kuwapa ajira na vile vile kuwapa ufundi ambao unahitajika katika kila sehemu. Kuna sehemu zingine ambazo zina ufundi maalum. Kwa mfano ukienda Lamu utapata kwamba fundi wa seremala wale ambao wanatengeneza Lamu carvings zinatoa taswira nzuri sana ya Kaunti ya Lamu na vile vile inapeana nafasi ya utalii na kupata pesa nyingi kwa mifumo kama hiyo. Vyombo vinavyotengenezwa na ufundi kama huo vinagharimu pesa nyingi kwa sababu ya ule ufundi wa kuchonga ambao unaambatana na taaluma hiyo. Ufundi kama huu hauwezi kupatikana katika vyuo vya kisasa vya ufundi lakini inaweza kupatikana kwa wale ambao wameweza kuwa na taaluma ile kwa muda mrefu na wengi wao hawakuenda shule kufundishwa taaluma kama hiyo. Tukitoa nafasi kama hii ya vyuo vya kiufundi itawapa nafasi wale ambao wana taaluma kama hizo kuweza kuzipitisha kwa vizazi vifuatavyo. Naunga mkono Mswada huu na ninajua utasaidia pakubwa kwa kupunguza ukosefu wa ajira katika nchi yetu na vile vile pia kuleta maendeleo kwa sababu wale ambao watafundishwa watatumia ujuzi wao kusaidia kuinua uchumi wetu kwa njia mbali mbali na hiyo itakuwa faida kubwa ambayo tutapata kwa Mswada huu. Asante, Bi. Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii."
}