GET /api/v0.1/hansard/entries/1098758/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1098758,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1098758/?format=api",
    "text_counter": 200,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "Shukrani, Bi. Naibu Spika. Kwanza, ninampa kongole ndugu yangu, Sen. Kinyua, kwa kuleta Taarifa hii. Yeye ni Seneta mchapa kazi ambaye anawakilisha Kaunti ya Laikipia. Vilevile, ni mwenzangu katika kuzungumza Kiswahili mufti. Ni aibu kwamba leo hapa Kenya, jeshi letu haliwezi kuchukua hatua. Sasa hivi, tunavyoongea, familia 40 zimefurushwa kutoka makao yao huko Olmoran. Katika eneo la Kisii Ndogo, takrniban nyumba 50 zimechomwa na watu kufurushwa. Mkutano wa polisi ulikuwepo katika eneo hilo na kufanya mkutano mkubwa lakini huyu Bw. Natembeya na mkubwa wa polisi wa Kaunti ya Laikipia, wamezembea katika kazi yao. Kisii ndogo, kuna nyumba karibu 50 zimechomwa na watu kufukuzwa na wamehama. Ni jambo la aibu kwamba mkutano mkubwa wa maafisa wa polisi ulikuwa katika eneo hilo lakini huyu mtu anayeitwa Bw. Natembeya, amabaye ni Kamishna wa eneo hilo la Laikipia, amezembea katika kazi yake. Kama Kamishna huyo amechoka na kazi, afadhali atoke Laikipia na ampishe kamishna mwingine ambaye atachukua nafasi hiyo. Yeye ameshindwa na hiyo kazi. Bi. Naibu Spika, tunajua kuwa Seneta wa Kaunti ya Laikipia anaongea ukweli. Sijui kama yeye anaweza kuongea kitu ambacho si cha ukweli. Akisema kuwa Wakenya 50 walio na vitambulisho vya Kenya, wakenya halisi, wako na nyumba zao ilhali leo zinachomwa na mali zao zinaharibiwa, sisi tunamuamini. Wezi wa mifugo wamechukua mifugo ya watu ambayo wanategemea mifugo hao kuwapatia rasilimali kama maziwa. Wafugaji hao huuza nyama na kujikimu na mazao ya mashamba yao, lakini leo wamekuwa walala hoi ndani ya nchi hii. Hilo ni jambo la kulaumu na kudhalilisha familia ambazo zinateseka sana. Wanaoteseka zaidi ni kina mama ambao wanabeba watoto, wanao lala nje, wanalia kwa kuwa dhiki imeingia katika familia zao. Ni jambo la kusikitisha ya kwamba mambo haya tulisikia yakitokea lakini hakuna hata mmoja wetu katika Bunge hili alitafakari kama kitendo kama hiki kinaweza kutendeka ndani ya Kenya. Tunaona sasa katika inchi hii wakenya wakiwauwa wakenya wanzao. Kufikia sasa, watu wanane wamekufa ndani ya Kaunti ya Laikipia. Huyu mtu anayeitwa Natembeya anaketi pale na kusema kuwa hana uwezo, amekuwa run over, yaani amekanyagwa hadi hajiwezi."
}