GET /api/v0.1/hansard/entries/1098816/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1098816,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1098816/?format=api",
    "text_counter": 258,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Mwaruma",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13223,
        "legal_name": "Johnes Mwashushe Mwaruma",
        "slug": "johnes-mwashushe-mwaruma"
    },
    "content": "Pili, ninakashifu kwa kinywa kipana, matukio yanayopelekea watu wa Kaunti ya Laikipia kuteswa katika Karne ya 21, kwa sababu ya Serikali kushindwa kudhibiti hali ya usalama. Matamshi ya Mshirikishi wa eneo la Bonde la Ufa ni ya kuudhi na kukashifu. Alisema kwamba silaha za polisi wa Kenya ni za hadhi ya chini kuliko za wale wahalifu. Ningependa kumwambia Bw. Natembeya na Serikali kwa jumla kuwa kama hawana silaha za hadhi ya juu, swala sio kulilia vyombo vya habari. Wanatakiwa kutafuta hizo zana za hadhi ya juu na kupea jeshi la Kenya ili wadhibiti usalama katika jimbo la Laikipia."
}