GET /api/v0.1/hansard/entries/1098875/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1098875,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1098875/?format=api",
"text_counter": 317,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kwamboka",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 9246,
"legal_name": "Beatrice Kwamboka Makori",
"slug": "beatrice-kwamboka-makori"
},
"content": "Ninaomba Serikali ya Jubilee iharakishe kuwa inawasaidia watu wanaoumia kule Kaunti ya Laikipia. Maafisa wa polisi ambao wanatakiwa kusuluhisha jambo hili waende huko haraka ile waangalie nini kinachoendelea. Tunanyosha tu kidole kwa Waziri na wengineo lakini huu sio wakati wa kulaumiana. Tunapaswa kuwa na mkutano na kuona kwamba askari wamepelekwa huko ili waokoe maisha ya Wakenya. Iwapo kuna upungufu wa askari, ni vyema tuelezwe ili hali hii ishughulikiwe haraka ipasavyo kwa sababu mwaka ujao ni mwaka wa siasa na uchaguzi. Mambo yanayoendelea huko sio mazuri. Bi. Spika wa Muda, niko katika Kamati ya Usalama wa Nchi, Ulinzi na Mawasiliano ya Kimataifa na Mwenyekiti wangu yuko hapa. Atatueleza jinsi tutakavyolabiliana na swala hili. Ni muhimu twende huko kwa haraka tuangalie hali ilivyo ili watu wetu wasaidike."
}