GET /api/v0.1/hansard/entries/1098916/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1098916,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1098916/?format=api",
    "text_counter": 358,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "Asante, Bi. Naibu Spika, unajua wewe ni mwingi wa imani pia wewe ni mama na wanaoumia zaidi katika janga la njaa ni akina mama. Ninamshukuru ndugu yangu kwa kuleta hii Taarifa kuhusu janga la njaa nchini, hususan akigusia upande wake wa Kaunti ya Kitui. Ni kweli kuwa kuna maeneo yaliyotangazwa kwamba yamo hatarini kuathirika na janga hili la njaa. Miongoni mwa kaunti hizi ni Kitui, Garissa, Kilifi, Mandera na kwingineko. Janga la njaa linapotokea, watoto wa shule na akina mama ndio wanaathirika zaidi. Wazee hawaendi shambani wala hawashughuliki na watoto na haya yote ni mzigo. Mama amebeba mtoto mgongoni huku anatafuta kuni. Ni mama ndiye anapikia mtoto asubuhi kabla mtoto kwenda shule. Mama anashughulika na mambo mengi. Bi Spika wa Muda, ni vizuri kwamba Rais amesema kuwa hili janga la njaa lishughulikiwe vilivyo. Wizara ya Ugatuzi na Mipango, wapeleke chakula haraka iwezekanavyo katika maeneo yaliyotajwa kuathirika sana na njaa. Tunasikitika kuona mifugo wanakufa kwa kukosa maji. Hivi sasa, mifugo wanakufa kwa sababu hakuna mito ambayo inatoa maji na visima vimekauka. Mifugo inakufa na hiyo ndio faida ya watu wanaishi katika maeneo ambayo yana upungufu wa mvua."
}