GET /api/v0.1/hansard/entries/1099071/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1099071,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1099071/?format=api",
    "text_counter": 72,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "Bi. Naibu Spika, Sen. Prengei alitoka katika jamii la Ogiek ambao wanaishi katika Bonde la Ufa. Hii ni jamii ndogo sana tena ya watu wachache sana. Kumpoteza mtu kama huyu katika jamii na familia ndogo kama hiyo, sio jambo ambalo kila mtu anatafakari. Sisi tuko upande huu wa Bunge na yeye alikuwa ule upande mwingine wa wale waliomteua. Pale walipo, tunawaomba tu waangalie maswala ya jamii ya Ogiek. Lipo jukumu la kuhusisha hili kabila dogo la Ogiek, ili kupatikane kiongozi mwingine kutoka hii jamii, apewe nafasi hiyo kumaliza muhula huu unaoendelea hadi mwaka wa 2022. Mimi na watu wa Kaunti ya Kilifi tunasema pole kwa familia, jamii ya Ogiek an watu wa Bonde la Ufa. Maseneta tunasikitika na tunaomba Mwenyezi Mungu aiweke roho ya marehemu mahali pema peponi."
}