GET /api/v0.1/hansard/entries/1099090/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1099090,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1099090/?format=api",
"text_counter": 91,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Boy",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13200,
"legal_name": "Issa Juma Boy",
"slug": "issa-juma-boy"
},
"content": "Asante sana, Bi Naibu Spika, kwa kunipa fursa hii. Kwa niaba yangu na watu wa Kaunti ya Kwale, natoa rambirambi zangu kwa familia ya mwendazake Sen. Prengei. Marehemu alikuwa Naibu Mwenyekiti katika Kamati ya Ardhi, Mazingira na Mali ya Asili. Ninakumbuka kabla hajatoka katika Kamati ile, tulikuwa na matembezi ya Kaunti ya Kwale. Tuliandamana na yeye na Kamati yote kwenda kuangalia mzozo wa ardhi Diani, Mbela Farm na uwanja mdogo wa ndege wa Ukunda. Katika mazungumzo yake kama Naibu Mwenyekiti wetu, alikemea sana watu ambao wanaochukua ardhi ya watu na kudhulumu wananchi. Machozi yanatulenga tukikumbuka marehemu Sen. Prengei akitetea haki za wananchi. Sisi kama wanadamu hatuna la kusema bali kumwombea Mwenyezi Mungu alaze roho yake mahali pema peponi. Sisi kama Maseneta tukumbuke familia yake kwa sababu ana watoto wadogo. Lazima tutafute wakati kwenda kuwafariji. Kwa hayo machache, asante sana."
}