GET /api/v0.1/hansard/entries/1099095/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1099095,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1099095/?format=api",
    "text_counter": 96,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Omanga",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13175,
        "legal_name": "Millicent Omanga",
        "slug": "millicent-omanga"
    },
    "content": "Asante Bi. Naibu Spika kwa kunipa fursa ya kumwomboleza mwendazake, ndugu yetu, Sen. Victor Prengei. Alikuwa kijana mdogo shupavu ambaye alikuwa katika ujana wake. Alikuwa pia rafiki wa karibu. Nilikuwa kwenye kamati ambayo ilifanya maandalizi ya sherehe yake ya mwisho. Tulikuwa naye kwenye Kamati ya Delegated Legislation . Ni mtu aliyependa watu wake sana. Tulipokuwa na Mswada kuhusu watu wake, vijana ama jamii ndogo, alikuwa na roho ya kufanya jambo. Tulisumbuka naye sana kwenye chama chetu cha Jubilee. Alikuwa Mariashoni kule Elburgon na akapata ujumbe mfupi wa kumwalika aende mkutano. Wengi wetu ambao tulienda huko kwenye sherehe yake ya mwisho tuliona ya kwamba hakuna mtandao na kwa hivyo angeweza kupata ule ujumbe. Kwa sababu angeweza kufika, chama chetu kilimdhulumu sana. Alikuwa na wasiwasi na ikawa ngumu kwake kufanya kazi. Alikuwa anapata vitisho na hangekaa kwa amani. Karibu apate ugonjwa kwa sababu ya vitisho alizopata kwa kukosa kuhudhuria mkutano huo. Lakini alisimama kidete na kile alichoamini kwamba hakupata ule ujumbe na ndio sababu hakuenda kwa mkutano. Kwa sababu hiyo, tulienda kortini na tuna kesi hadi wa leo. Tuliangaishwa kama Jubilee Six. Alitumia pesa nyingi kortini kwa swala ambalo alikuwa la maana. Alikuwa kijana ambaye alipenda kujihusisha na kila mtu katika Seneti. Wakati tulikuwa na sherehe yake kanisani, ulisimama na kusema vile ulivyomjua. Ilitushangaza"
}