GET /api/v0.1/hansard/entries/1099145/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1099145,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1099145/?format=api",
    "text_counter": 146,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "Asante, Bw. Spika wa Muda. Kwanza, ninamshukuru ndugu yangu, Sen. Khaniri, kwa kuleta Ardhilhali hii. Tunajua mambo ya mashamba yako na utetesi mwingi. Tunaelewa kwamba watu wetu hupata riziki yao kutoka mashamba yao na wanapenda kuyamiliki. Hapo zamani palikuwa na mwanasiasa kwa jina J.M. Kariuki kutoka Kaunti ya Nyandarua. Katika hili Bunge, alisema kwamba Kenya ilikuwa na matajiri elfu kumi na masikini millioni kumi. Hilo lilikuwa jambo la kusikitisha lakini yeye alikuwa upande wa Kaunti ya Nyandarua na aliongea juu ya Wakenya wengi. Hivi leo, kama kuna donda sugu ni suala la uskuota nchini. Mashamba ya ADC yamejaa maskuota. Tunavyoelewa hatupaswi kuwa na maskuota kwa sababu sisi sote ni Wakenya. Ni jambo la aibu sana kwa kwamba hata sheria zetu, hakuna mtu ambaye ni skuota. Hapa tumebuni neno ‘skuota’ kuwataja watu ambao hawana hati za kumiliki ardhi zao watu wasioishi Kenya. Ardhi hii iko katika Kaunti ya Nandi ya ndugu yangu mdogo, Seneta mshupavu naninamuezi sana. Ninatumaini yeye mwenyewe analiifikiria jambo hili na atachukulia hatua ya nguvu zaidi. Ndugu yangu usilegeze kamba kwa sababu watu wa Kaunti ya Nandi wanakuhitaji. Katika Kaunti ya Kilifi kuna shamba kubwa sana la ADC upande wa Sabaki. Hilo shamba lina historia na lilipeanwa kwa wananchi wenyewe. Zipo taratibu na stakabadhi nyingi sana ambazo ziliandikwa na viongozi waliokuwa Serikalini wakati huo, wakiesema shamba hilo lirejeshewe watu wanaoishi eneo la Magarini, hususan wanaoishi Sabaki. Lakini ufisadi mkubwa ulitokea baada ya mabwanyenye kujitokeza. Mwakilishi wa Wadi hiyo kwa jina Mhe. Bele, alikuwa akiuliza maswali na kuhoji na kutembelea watu wa huko kuona kwamba wako sawa. Mhe. Bele alikamatwa na kutiwa mbaroni. Mimi pamoja na mawakili wengine tulimtetea na akaachiliwa huru. Hili shamba la ADC katika eneo la Magarini sehemu ya Sabaki linatuhusu sana. Haki za Wagiriama na Wakenya wengine walipewa hati miliki ya hayo mashamba na wakaenda kuishi hapo. Hata hivyo, haki zao zilikiukwa kwa sababu walifurushwa na kuondolewa kinyama. Iwapo Serikali ina Wizara hususan inayohusika na mambo ya mashamba, ni jambo la kusikitisha kuona watu wamejikunyata mahali pamoja ilihali shamba walilopewa na Serikali liko hapo. Ni lazima Serikali iamuru watu hawa warejeshwe katika ardhi yao ya ADC huko Sabaki na waruhusiwe kuitumia ardhi hiyo kama makao yao na waweze kujikimu."
}