GET /api/v0.1/hansard/entries/1099295/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1099295,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1099295/?format=api",
    "text_counter": 296,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "Kipengele cha Katiba cha 219 kinashurutisha kikisema kwamba bila kupoteza wakati ama muda wa kisawa sawa unaotakikana ama bila kuchelewesha hizi pesa, pesa hizi zinatakikana zitolewe katika Hazina ya Kitaifa na ziende katika serikali za mashinani. Je, huu ni ukiukaji wa Katiba? Kama ni ukiukaji wa Katiba wa kweli kulingana na Kipengele cha 219 kinachosema pesa hizo “ without undue delay,” yaani bila kuchelewesha kwa muda ambao hautakikani. Pesa hizi zinatakikana zifike katika serikali za mashinani. Tunauliza yeye awezekupeleka hizi pesa. Bw. Spika wa Muda, ni jambo la aibu kufikia hivi sasa ya kwamba Waziri wetu wa Hazina ya Kitaifa ako na Kshs62 bilioni mikononi mwake na bado hajazipeleka katika kaunti zote 47 ikiweko Kaunti ya Samburu ambayo Bw. Spika wa Muda wewe ni mwakilishi ndani ya hii Seneti. Ukiwa unawakilisha watu wa Kauti ya Samburu, hawajapata mgawo wao wa pesa. Tunasema watu wa Kaunti ya Samburu pia wana haki ya kupewa hizo pesa zao ili wapate kufanya maendeleo. Kama ni madawa, akina mama, watoto na wazee wasiojiweza wapate na manufaa yawezekufika katika serikali zile za huko mashinani. Ni aibu kubwa kwa Serikali yetu ya Kenya kuona ya kwamba hizi pesa zimeweza kuzuiliwa ndani ya serikali. Hatujui hizi pesa zinafanya nini pale ndani ya ofisi ya Waziri wa Hazina ya Kitaifa. Bw. Spika wa Muda, Mswada huu ni muhimu sana kuliko Miswada yote. Tunasema hili Seneti liko hapa kwa sababu ya ugavi wa pesa. Watu walikuwa wakitishwa hapa. Tulikuwa tukitishwa hapa hata kutiwa ndani. Wenzetu walifungwa. Wengine walikuwa katika maeneo yao wakiwa wanataka kuja hapa ndani ya Bunge ili kupitisha Mswada kama huu ambao ulikuwa unajulikana ni hatari. Wewe ni mmoja wao. Ulinaswa barabarani ukiwa ndani ya gari lako ukatolewa ukatiwa ndani ya lori. Ukapelekwa mpaka kwa polisi. Seneta wa Kaunti ya Kakamega alishikwa na kuwekwa ndani. Kuna Maseneta wengine walinyanyaswa. Sisi wengine tukatishiwa maisha kwamba tunawezakupigwa risasi. Tukasema kama mnaweza kupiga risasi; pigeni kwa sababu ya Mswada huu. Lakini jambo la kusikitisha ni kwamba hapa ndani tuko watu saba tu ukiangalia. Maseneta 40 wako wapi? Bw. Spika wa Muda, Hoja kama hii inatakikana tujadiliwa hivi sasa na tupige kura ili tuweze kulazimisha Serikali kupitia Hazina ya Kitaifa na Waziri ili Mswada huu upewe kipaumbele. Halafu pesa hizi zote ambazo zinatakikana kupelekwa katika serikali za mashinani ambazo sio chini ya Kshs62 bilioni ziweze kupatikana. Ombi langu ni kwamba pesa hizi ziweze kupelekwa katika serikali za mashinani haraka iwezekanavyo ili watu waweze kufaidika na mgawo wa pesa zao. Asante."
}