GET /api/v0.1/hansard/entries/110073/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 110073,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/110073/?format=api",
"text_counter": 407,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. M.Y. Haji",
"speaker_title": "The Minister of State for Defence",
"speaker": {
"id": 26,
"legal_name": "Yusuf Mohammed Haji",
"slug": "yusuf-haji"
},
"content": " Ahsante sana, Bw. Naibu wa Spika. Kwa muda mrefu, Kenya ni taifa ambalo limekuwa likijigamba eti linaheshimu demokrasia na lina umoja mpaka mwaka wa 2007 tulipokuwa na matatizo baada ya uchaguzi. Tangu wakati huo, inaonekana nchi hii imegawanywa kwa misingi ya kikabila, kidini na kisiasa. Ninasema hivyo kwa sababu ijapokuwa tumekuwa na Katiba kwa miaka zaidi ya 40, wengi waliozungumza hapa wamesema kwamba kwa muda wa miaka 20 tumekuwa tukipigana kubadilisha Katiba. Kama alivyosema Bw. Naibu wa Spika, Katiba ni karatasi. Kama chombo chochote kile, karatasi inaweza kutumika vizuri au vibaya. Hadi Wakenya watakapokubali kubadilisha mienendo yao, kwa mfano, kukataa kupeana rushwa, ukabila na kugawanya watu kwa misingi ya dini, hata Katiba hii irekebishwe mara 1,000, hakuna faida yoyote italeta nchini. Mimi nimetumikia nchi hii kwa miaka 40. Nimefanya kazi katika matarafa ambamo hata Waislamu hawafiki 12 lakini hakuna hata siku moja nimebaguliwa kwa"
}