GET /api/v0.1/hansard/entries/110075/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 110075,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/110075/?format=api",
"text_counter": 409,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "kuwa mimi ni Mwislamu wala sikubagua mtu kwa sababu ya dini yake. Ni jambo la kustaajabisha kwamba kipengele kinachohusu korti za Kadhi kilipitishwa huko Bomas of Kenya na Wakenya zaidi ya 600 waliotoka katika kila wilaya. Vile vile, kulikuwa na Wabunge 210 wakati majadiliano yalikuwa yakiendelea. Hicho kipengele kilipigiwa kura na ijapokuwa Waislamu ni wachache wakilinganishwa na wananchi wengine, kati ya zaidi ya watu 347 waliopiga kura, watu 237 waliunga mkono mambo ya korti za Kadhi. Pia, kipengele kinachohusu korti za Kadhi kilipitishwa katika Wako Draft. Isitoshe, Kamati ya Wataalamu wameidhinisha korti za Kadhi. Wabunge walipokuwa Naivasha walikubaliana kwamba suala la korti za Kadhi halidhuru Mkristo, Baniani au kafiri. Jambo la kushangaza ni kwamba baada ya zaidi ya miaka 40 tumejitawala, mbona watu wameamka leo kupinga korti za Kadhi? Hili ndilo jambo linalonifanya niseme kwamba kuna watu ambao wanataka kuleta uhasama miongoni mwa Wakenya kwa misingi ya kidini. Sisi hatukubaliani na mambo haya. Ninawaomba wale ambao wana fikira kama hizo waachane nazo kwa sababu hatutaki kitu ambacho kitadhuru umoja ambao tumekuwa nao miaka hii yote."
}