GET /api/v0.1/hansard/entries/110078/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 110078,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/110078/?format=api",
    "text_counter": 412,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Haji",
    "speaker_title": "The Minister of State for Defence",
    "speaker": {
        "id": 26,
        "legal_name": "Yusuf Mohammed Haji",
        "slug": "yusuf-haji"
    },
    "content": " Ahsante, Bw. Naibu wa Spika. Hakuna mtu ambaye amesema kwamba Katiba tuliyo nayo leo imefanya jambo hili na lile. Ninasema hivyo kwa sababu wenye kufanya mambo ni watu binafsi. Wao ni Wakenya ambao walikuwa kwenye madaraka. Katiba haijaharibu kitu. Isitoshe, Katiba mpya inayopendekezwa ina vipengele vingi ambavyo vikipitishwa vitaweza kuleta moto katika nchi hii. Kuna kipengele kinachohusika na usalama ambacho kinasema kwamba kila mtu ana haki ya kuadamana. Kuna kipengele vile vile ambacho kinasema kwamba Bunge linaweza kurekebisha hicho kipengele kwa kuunda sheria ya kuyatoa majeshi, polisi na maofisa wa jela. Ikiwa kwa bahati mbaya Bunge linavunjwa ama linakwenda mapumzikoni kabla ya kutengeneza hiyo sheria, nani atazuia majeshi ama polisi kujiunga na maandamano? Hii ni kwa sababu Katiba hii inayopendekezwa inapeana huo uhuru. Kuna kipengele kinachosema kwamba mwanajeshi ana haki ya kuchukua wakili amwakilishe katika kesi ndogo. Kwa mfano, ikiwa kuna meli ya jeshi baharini nayo inaelekea vitani na kuwepo na askari mmoja ambaye atakosea, basi Mkuu wa hiyo meli ataweza kumwadhibu. Lakini tukifuata hii sheria inayopendekezwa, italazimu meli irudi itie nanga ndiposa huyo mwanajeshi atafute wakili. Je, hii ni sheria nzuri kwa nchi hii? Sidhani hivyo. Kwa hivyo, mimi ninaomba Bunge hili liangalie vile vipengele ambavyo vinaweza kuleta taabu katika nchi hii ili tuvibadilishe."
}