GET /api/v0.1/hansard/entries/1101503/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1101503,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1101503/?format=api",
"text_counter": 204,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "askari hao wanakuwa waoga. Sasa ikiwa askari wanaogopa kufuata wahalifu hao, ni kina nani watafuata kule ndani? Uvamizi kama huu na watu ambao wanaiba mifugo, kuua watu na kuleta maafa na kuharibu mali ya watu, Serikali inatakikakana kupambana nao vilivyo. Kamati ya Usalama inatakikana iende huko mara moja kuonyesha kwamba sisi tunafanya kazi na tunawajali wananchi. Kamati hiyo inafaa iende huko na ilete ripoti haraka iwezekanavyo ili tuweze kuona ya kwamba amani imepatikana katika eneo hilo la Laikipia. Laikipia ni Kenya; haiko nje ya Kenya. Kwa hivyo, ni lazima iangaliwe kisawasawa. Hatusemi wanajeshi watumwe katika eneo hilo. Tungependa maaskari watumwe pale ili kudumisha amani. Hatukaki wanajeshi watumwe pale---"
}