GET /api/v0.1/hansard/entries/1101561/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1101561,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1101561/?format=api",
"text_counter": 262,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mwaruma",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13223,
"legal_name": "Johnes Mwashushe Mwaruma",
"slug": "johnes-mwashushe-mwaruma"
},
"content": "wanaojitafutia kipato na wazee na kina mama wanaolima shambani bila barakoa. Hatuhitaji maaskari kama hao kule Kaunti ya Taita-Taveta. Wapelekwe Laikipia kuangalia hali ya usalama. Katika Karne ya 21 haitakikani tuwe na economic activity ama njia ya kujitafutia kipato kupitia kuiba ng’ombe. Tuweke elimu mbele, tuangalie njia mbadala na tufanye utafiti wa kutosha ili jambo hili la wizi wa mifugo liishe mara moja. Kwa kumalizia, tuite hizi taasisi zote za usalama ili tuwaulize maswali magumu hapa katika Seneti na tuwe na kamati ya Bunge zima . Tukiuliza maswali rahisi maisha ya watu wa Laikipia yatakuwa magumu. Lakini tukiuliza maswali magumu, basi Maisha ya watu wa Laikipia yatakuwa rahisi. Asante sana, Bi Spika wa Muda."
}