GET /api/v0.1/hansard/entries/110180/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 110180,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/110180/?format=api",
"text_counter": 514,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Mwadeghu",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 98,
"legal_name": "Thomas Ludindi Mwadeghu",
"slug": "thomas-mwadeghu"
},
"content": "Bw. Naibu Spika, naomba nichangie Hoja hii ya Katiba ili nami nitoe maoni yangu kuhusu Katiba ambayo natarajia Wakenya wanaitaka. Je, Katiba hii ni ya nani? Je, Katiba hii inanuia nini na inatuongoza wapi? Je, Katiba hii inatililia maanani haki za wananchi? Nitaanzia baba zetu ambao walienda Lancanster miaka hiyo ya awali. Nawashukuru. Nawasifu pia hawa wataalamu wetu ambao tuliwachagua hapa kwa kazi nzuri waliofanya. Pia nawashukuru Wabunge wenzetu 27 kwa kazi ambayo wamefanya mpaka tukapata Katiba kielelezo. Katiba hii kielezo ambayo tuko nayo hivi sasa ni nzuri nikilinganisha na ile inayotuongoza wakati huu. Kwa hivyo tukishindwa kuelewana kama Wabunge kwa vipengele ambavyo labda huenda vikahitaji kugeuzwa, basi Katiba hii kielelezo ipitishwe vile ilivyo. Bw. Naibu Spika, naomba kuchukua nafasi hii kuwashukuru wenzangu ambao wametoa maoni yao. Nilimsikia Prof. Saitoti akisema kwamba amekaa hapa kwa muda na pia Waziri wa Kawi akikiri dhahiri kuwa amejifunza mengi kutoka kwa wale wenzetu ambao wamenyanyaswa. Bw. Naibu Spika, wamejifunza uvumilivu kuwa kuna watu ambao wamenyanyaswa kwa muda mrefu sana na hadhi yao ilikuwa haiwekwi maanani na wenzetu. Hivyo basi, Katiba ya 1963, ikaanza kugeuzwa. Ilipogeuzwa, ni nini kilichotokea? Haki za wenzetu zilianza kuondolewa, moja kwa moja. Wakenya wakaanza kuulizana, nini kimetokea? Hapo, mori wa kutaka Katiba nyingine ukaanza kuingia na"
}