GET /api/v0.1/hansard/entries/110182/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 110182,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/110182/?format=api",
"text_counter": 516,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "mbegu ya chuki ikaanza kupanda na kuota wakati huo. Tusipokuwa waangalifu, hapa pia tutapanda mbegu ya chuki. Hiyo mbegu iliyopandwa iliendelea. Mwaka wa 1997, tukawa na uchaguzi. Uchaguzi huu ulikuwa na hitilafu. Wakenya wengi walikasirika lakini hawakuwa na namna ya kuweza kugeuza na wakayabana. Mwaka wa 2002, hali ilikuwa kama ile ya 1997. Watu waliumizana na kuuwana. Chuki ikaendelea kumea mizizi. Uchaguzi wa 2007, wenzetu wamekiri dhahiri hapa kama wangekuwa wamegeuza Katiba, labda haya maafa hayangewapata Wakenya. Swala nyeti ni hili: Kwa nini walishindwa kuigeuza Katiba wakati huo? Ni kwa sababu mara nyingi walikuwa na ubinafsi. Huo ubinafsi, hivi leo umedhihirika kwa waheshimiwa Wabunge. Kila mhe. Mbunge akisimama hapa anafikiria upande wake. Katiba kielelezo hii ni nzuri sana na ikiwa tutashindwa kugeuza vipengele, basi tuipeleke kwa wananchi kama vile ilivyo. Msimamo wangu ni kuwa ugatuzi au mfumo wa majimbo, hautaleta shida. Tunasema Rais ana mamlaka ambayo ni ya kiimla. Haya mamlaka yameletea nchi hii shida, tukianzia na Rais wetu wa kwanza. Alichukua mamlaka ya kiimla baada ya kuondoa Katiba ya mwaka wa 1963. Rais aliyefuata alikamilisha kuhakikisha kwamba imla imekita mizizi. Ilikuwa hamuwezi kufanya lolote bila yeye kujua. Watu wa Pwani wanapendekeza majimbo kwa sababu ya kunyimwa haki zao. Ilikuwa ni haki gani kwa watu kutoka sehemu nyingine, kuja na karatasi wanazoita âtitle deedsâ na kunyakua mashamba yetu? Walitimua watu wetu kutoka mashambani yao na kusema ni yao. Hapo mbegu ya chuki ilipandwa wakati huo na uoga ukaanza kuingia. Hivi sasa tukisema tunataka ugatuzi wa mamlaka, watu fulani wanashikwa na uwoga. Wengine wanadhani watu fulani watafukuzwa kutoka sehemu wanamoishi wakati huo au watu watafukuzana. Jambo hili si kweli. Tunataka kupeleka mamlaka kwa wananchi mashinani. Tunaomba tuwe na ngazi tatu za mamlaka. Tuwe na Rais, Senate na Serikali za Mitaa. Tukifanya hivyo, tutakuwa tumemaliza tatizo hili. Tatizo la ardhi ni lazima lishughulikiwe kwa undani zaidi. Wenzetu ambao wana matatizo ya ardhi ni lazima wafikirie. Tangu hapo awali, wenzetu wa northern frontier walikuwa hawajihisi kuwa wao ni Wakenya. Hivi sasa wanajihisi kuwa Wakenya kwa sababu wamepigania haki yao kwa muda mrefu. Tusidanganyane kuwa hatuna uwoga. Uwoga upo lakini sisi tukishirikiana, tunaweza kuumaliza uwoga huu. Naomba pia kipengele ambacho ni cha kutoa mimba kiangaliwe kwa makini. Sikubaliani nacho. Makanisa nayo yawe wazi na yaseme ukweli. Tunachangia shughuli za kutoa mimba zisikubaliwe kwa sababu ni hatia kuavya au kutoa mimba. Nakubaliana nao. Lakini kwa nini tusiwafundishe watu wetu tabia nzuri ili waepukane na mimba ikiwa hawako tayari kuanzisha maisha ya familia? Kwa nini sasa tunajishughulisha na suala hili? Kwa nini tuzozane juu ya jambo hili? Naomba niweke tamati kwa sababu wenzangu wana nia ya kuzungumza. Nikizungumzia mambo ya Mahakama---"
}