GET /api/v0.1/hansard/entries/110204/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 110204,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/110204/?format=api",
    "text_counter": 538,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Joho",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 30,
        "legal_name": "Hassan Ali Joho",
        "slug": "hassan-joho"
    },
    "content": "Ninatoa shukrani, Bw. Naibu wa Spika, kwa kunipatia nafasi hii. Kwanza, ningependa kutoa shukrani za dhati kwa Kamati ya Bunge (PSC) ambayo ilikuwa ikisimamia shughuli hii ikiongonzwa na Bw. Abdikadir na naibu wake, Bw. Ababu Namwamba, kwa kutupatia sifa kama Bunge la Kumi. Kiu cha kutaka Katiba mpya kimesababishwa na sababu nyingi. Zipo sababu ambazo ni msingi katika shughuli hii. Sababu muhimu ni uwakilishaji na utenda kazi wa Serikali kwa wananchi. Wale waliopigania kuwepo kwa Katiba mpya walikuwa wanataka mabadiliko katika Katiba. Mimi nikiwa mwakilishi wa watu, ninasema kwamba tumeanza safari ijapokuwa kumekuwa na safari za kibinafsi awali. Sasa tumeanza safari ya utendeji haki kwa Mkenya yeyote mahali popote alipo. Wakati tunapoingia katika kumbukumbu za kihistoria kwa kuzaa mtoto anayeitwa “Katiba Mpya” kwa niaba ya Wakenya, ni lazima tuwe na uwezo wa kulea kizazi hiki kipya. Bw. Naibu wa Spika, hii siyo Katiba ya karatasi. Ningependa tufahamiane na wenzangu na niwasihi vile vile. Uundaji Katiba si kuiandika. Tulipokuwa na uchaguzi mwaka wa 2007, tulikuwa na Katiba. Tulikuwa na sheria lakini bado maisha yalipotea. Kuwa na Katiba na kuiamini ni mambo mawili tofauti. Hii ndiyo maana tukasema kwamba kando na kazi nzuri ambayo imetendwa na Wakenya katika Kamati ya"
}