GET /api/v0.1/hansard/entries/110206/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 110206,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/110206/?format=api",
    "text_counter": 540,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Wataalamu (CoE) na Kamati ya Bunge (PSC), ni muhimu Katiba hii ilete kielelezo ambacho kitakomboa maisha ya Wakenya na kuweka mipango pamoja na utendakazi kidete, hali ambayo itaweka dhuluma katika vitabu vya historia. Wengi wamezungumza hapa kuhusu majimbo. Kuna wale ambao wamesema eti majimbo ina maana ya “kusafisha” makabila fulani kutoka katika maeneo yasiyokuwa yao. Ningependa kunukuu sheria za nchi jirani. Kwa mfano, nchi ya Ethiopia ina mikoa tisa. Nchi hiyo ina makabila 82 na serikali za mikoa. Sasa hivi, katika nchi zinazoendelea haraka kiuchumi, nchi ya Ethiopia haiwezi kuachwa inje. Hii ni kwa sababu ya kuwa na miundo-msingi mizuri, serikali za mikoa zinazoshindana, pamoja na kupanua nafasi za uwekezaji katika maeneo hayo. Bw. Naibu Spika wa Muda, si haki kuwa katika Bunge na kukosa kusema kwamba shida ya Bunge hili, ama shida ya uendeshaji Serikali katika nchi hii, ni kukata mamlaka na kuwapelekea watu wajiamulie ni haki gani wangependa. Hatuwezi kupitisha katiba, kwa sababu Katiba Kielelezi hiki ni kitabu tu tunaandika ili iende mbele ya Wakenya. Sisi ni viongozi tulioletwa hapa kuwakilisha Wakenya. Tumeletwa hapa kwa sababu ya matakwa ya watu wetu. Jambo moja la msingi la kuwaleta viongozi hapa ni kuweza kuzungumzia vitendo na mambo yanayoweza kunyoosha maisha ya mwananchi. Katiba Kielelezi inazungumzia suala la kubuniwa kwa National Land Commission. Sisi tunaonelea kwamba huko ni kuongezea ama kuugawanya ule utaratibu ulioko sasa. Ikiwa tunazungumzia ugavi wa mamlaka na kupelekea uwezo wananchi, ni lazima tuwe na Serikali ya msingi wa majimbo itakayoangalia ni namna gani tunaweza kugawa rasilmali, na ni namna gani tunaweza kukuacha wewe ujimudu kwa rasilmali ya chini kabisa, ambayo ni ardhi, na nyinginezo. Bw. Naibu wa Spika, ninataka nizungumzie juu ya Mahakama ya Kadhi kidogo, na niwasihi ndugu zangu wasiokuwa Waislamu kwamba, sisi katika Bunge hili la Kumi tuko katika mtihani mkubwa. Tusipelekwe na vitendo vidogo vidogo vya kando kando. Historia iko. Ninataka mkae mjiulize: Mahakama ya Kadhi iliingia vipi katika Katiba iliyoko sasa? Historia inasema nini kuhusu suala hili? Kulikuweko na mazungumzo gani? Je, hiyo ni demokrasia iliyopita? Ukanda wa Pwani ulikuwa chini ya Ufalme wa Uzanzibari. Mazungumzo yakafanyika, na ikakubalika kwamba Mahakama ya Kadhi yawekwe kwenye Katiba kulinda haki za ndoa na urithi wa Muislamu. Ninawasihi ndugu zangu, tusianguke mtihani tukiwa katika Bunge la Kumi. Tusifuate mambo ya kando kando na kuacha yale mambo ya koo na kiini cha nchi hii. Bw. Naibu wa Spika, ninataka kuwapa nafasi Wabunge wenzangu ili nao wachangie. Kwa hayo machache, ninaiunga mkono Hoja hii."
}