GET /api/v0.1/hansard/entries/1102317/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1102317,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1102317/?format=api",
"text_counter": 201,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Asante Bw. Spika wa Muda. Ninamshukuru Sen. Kasanga kwa kuleta Taarifa hii. Walemavu wanateswa kwenye kazi hizi. Ni jambo la aibu kwamba ukiendesha gari, mataa yakiwaka nyekundu, wanakuja kwa dirisha kuomba. Hili sio jambo linalotendeka katika barabara pekee. Siku hizi, wako katika vichochoro pia. Ukichunguza sana utaona kuna matajiri ambao waliwaleta kwenye barabara kuja kuomba omba ili wapate pesa. Nilikuwa nimeketi mahali fulani nanikaona mlemavu akiomba na baadaye ukimwachia pesa, baada ya dakika mbili au tatu, mtu anakuja kuchukua hiyo pesa na yeye anabaki pale pale. Hao ni wale wanaambiwa enda uketi pale ukichanga pesa kiasi fulani jioni tutakupa kiasi fulani. Bw. Spika wa Muda, ingekuwa vizuri ikiwa Serikali yetu itachukua uchunguzi maalum na wa kisawa. Kamati ya mambo ya utekelezaji wa wafanyikazi na mambo ya jamii iangalie zaidi na kufanya uchunguzi ili tuweke mapendekezo."
}