GET /api/v0.1/hansard/entries/1102408/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1102408,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1102408/?format=api",
    "text_counter": 292,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "Bw. Spika wa Muda, asante. Kwanza, nataka kujiunga na Maseneta wenzangu ambao wameweza kuchangia mjadala huu. Kama kuna kitu kikubwa ambacho watu wanaweza kukosania ni hali ya pesa. Tukiwa tunaongea mambo ya ugavi wa pesa zinazokwenda katika kaunti, hapo ndipo mahali watu huanza kukosana. Nakumbuka wakati ule wa ugavi wa pesa, Maseneta kutoka pande zote mbili, kama vile alivyosema ndugu yangu, Sen. Murkomen. Tuliweza kujitenga na kusema kwamba inafika wakati mtu anafikiria, je, ni kaunti yangu ama ni njia nyingine panda? Tunasema kwamba kila Seneta hapa aliyekuwa anapoteza na hata wale ambao walikuwa hawapotezi walikuwa na imani sana kwamba katika taifa la Kenya, haina haja ionekane wengine watapata zaidi na wengine kidogo ama wengine watapunguziwa na wengine wataongezewa. Ilikuwa ni sharti tuone ya kwamba haki ya ugavi wa zile pesa ilikuwa inaenda sambamba vile Wakenya wanataka. Bw Spika wa Muda, ukiangalia hivi sasa, wale wauguzi katika Kaunti ya Mombasa, katika hospitali zote za serikali, wamegoma na hawafanyi kazi. Wamegoma na hali hiyo inaweza pia kuathiri wale wagonjwa ambao wanaenda kutafuta matibabu. Yote"
}