GET /api/v0.1/hansard/entries/1102410/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1102410,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1102410/?format=api",
    "text_counter": 294,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "haya yanaletwa kwa sababu pesa hizi hazijafika kwenye serikali za mashinani. Ni jambo la aibu hivi sasa ikiwa tumeketi hapa na wauguzi katika Kaunti ya Mombasa wamesusia kazi. Wanasema hawawezi kufanya kazi kwa sababu utafanya kazi aje ikiwa tumbo lako liko na njaa? Tuko na Maseneta kwenye kamati hapa. Dadangu, Sen. Kwamboka, na ndugu yangu, Sen. Olekina; ndugu zangu Maseneta, sioni sababu ya kwamba Mombasa ama mahali popote katika nchi hivi sasa wamesusia kazi. Sen. Olekina, tafadhali angalieni haya mambo mkiwa katika Kamati ya Afya. Endeni mashinani na Hazina ya Kitaifa na katika wizara muone kwamba pesa hizi zimetolewa na zimeenda mashinani ili kuwasaidia wale dada zetu wapate mishahara yao ili waendelee kujikimu kimaisha. Bw Spika wa Muda, hili ni jambo la kusikitisha. Mhe. Yatani yuko pale kama Katibu wa Baraza la Mawaziri katika Wizara ya Fedha na hajatuma hizi pesa katika serikali zetu mashinani. Basi haina budi isipokuwa hili Seneti kujitambulisha na kuona kwamba ikiwa Seneti imepitisha, basi kuna umuhimu wa Seneti iende katika Mahakama Kuu ili kuona kwamba uamuzi umetolewa kama itakuwa ni sawa ama sio sawa Mhe. Yatani apelike hizi pesa katika serikali zote 47 za mashinani. Tulipitisha sheria ya County Revenue Allocation Act (CARA) tarehe 30/6/2021. Baada ya siku 15 tukishapitisha bajeti, pesa hizi zinafaa kupatikana na kupelekwa katika serikali za “ mashetani”, hapana za mashinani. Sio serikali za mashetani, ni serikali za mashinani. Nataka nieleweke vizuri. Serikali za mashinani. Isije ikaleta kizungumkuti bure. Bw. Spika wa Muda, nataka kuuliza ikiwa Waziri wa Fedha, Mhe. Yatani anajua kwamba hizi pesa kutokea tulipopitisha sheria hii tarehe 30/6/2021 inampa siku 15 ili aweze kupeleka hizi pesa zote katika serikali za mshinani na hajafanya hivyo, basi hili Bunge lingejitamka lenyewe. Inawezakuchukua hatua na kumwambia Mhe. Yatani awezekupeleka hizi pesa katika serikali za mashinani. Bw. Spika wa Muda, nikija upande wa watu wa Kaunti ya Kilifi. Serikali ya Kaunti ya Kilifi bado haijapata mgao wa pesa uliopelekwa. Mwezi wa Saba; ilikuwa wapate Kshs931 milioni. Hawajapata hata ndururu. Mwezi wa Nane ambao tumeachana nao hivi sasa ilikuwa wapate Kshs989 milioni. Kufikia hivi sasa Mwezi wa Tisa wanatakikana wapate Kshs989 milioni. Ukijumuisha pesa hizo zote wangepata Kshs2.9 bilioni. Huu ni uzembeaji wa kazi ya Mhe. Yatani ama kuna kizungumkuti gani kinafanywa hapo mpaka hivi sasa pesa hizi ambazo zinatakikana kutumika ndani ya Serikali ya Kaunti ya Kilifi hazipo? Pesa hizi zingesaidia kuleta maendeleo na kupeleka madawa katika hospitali zetu na vifaa vingine vinavyotumiwa na wananchi. Mpaka hivi sasa, pesa hizi hazijakwenda katika Serikali ya Kaunti ya Kilifi. Tunauliza, je, ni haki kutendea Kaunti ya Kilifi namna hii? Kama Mhe. Yatani anaweza kuzuia hizo pesa, tunamwambia sasa hivi, hili Bunge lishapitisha na tumeshatamka kwamba pesa hizi Kshs2.9 bilioni zinatakikana kwenda katika Serikali ya Kaunti ya Kilifi. Vile vile, katika serikali zote za ugatuzi katika Kenya ambazo hazijapata hizi pesa, ni sharti Mhe. Yatani aweze kupeleka hizi pesa katika serikali za mashinani."
}