GET /api/v0.1/hansard/entries/1102500/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1102500,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1102500/?format=api",
    "text_counter": 69,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Endebess, JP",
    "speaker_title": "Hon. (Dr.) Robert Pukose",
    "speaker": {
        "id": 1458,
        "legal_name": "Robert Pukose",
        "slug": "robert-pukose"
    },
    "content": "Hili jambo la bei ya mafuta kupanda linakera Wakenya wengi sana. Gharama ya maisha inaenda juu. Ukilinganisha bei ya mafuta katika nchi yetu ya Kenya na nchi jirani kama Uganda, Tanzania na Rwanda, iko juu sana hapa nchini. Nilimsikiza Kiongozi wa Walio Wengi akiongea na nilitaka kujua kwa nini bei ya mafuta Kenya iko juu kuliko bei ya mafuta katika nchi zingine. Inamaanisha kuwa nchi zile zingine hazina ushuru ama wao wanafanya nini? Tunatoa mafuta mahali pamoja. Hayo mafuta yanapitia Kenya yakipelekwa Uganda. Uganda inatumia gharama ya juu kupeleka mafuta nchini mwao kutoka Kenya. Kwa nini bei ya mafuta Uganda iwe chini kuliko bei ya mafuta hapa Kenya? Kule Uganda, lita moja inauzwa Ksh110 wakati lita moja hapa Kenya inauzwa Ksh135. Hilo ndilo swali ambalo watu wanajiuliza. Kwa hivyo, vile ulivyotoa amri, tunataka Kamati ambayo inaongozwa na Mhe. Wanga, ingawa hayuko hapa, na ninatarajia mahali alipo anafuatilia mjadala huu, ilete ripoti katika wiki mbili ambazo umewapa na Bunge hili liweze kujadili ili tuone kama tunasimama na Wakenya ama la. Wakenya wanalia sana. Walituchagua ili tuwawakilishe. Sisi kama wawakilishi wa Wakenya ni lazima tupate suluhisho ambalo litaleta gharama hii chini ili Mkenya wa kawaida aweze kuendelea na maisha yake ya kawaida."
}