GET /api/v0.1/hansard/entries/1102598/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1102598,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1102598/?format=api",
"text_counter": 167,
"type": "speech",
"speaker_name": "Igembe South, Independent",
"speaker_title": "Hon. John Paul Mwirigi",
"speaker": {
"id": 1574,
"legal_name": "Cyprian Kubai Iringo",
"slug": "cyprian-kubai-iringo"
},
"content": " Asante sana, Mhe. Spika. Pia nami naungana na wenzangu kuunga mkono Ardhilhali hizi mbili. Ukweli wananchi wameweza kuumia sana wakati ule ambapo bei ya mafuta ilipanda. Wakati huu wananchi wamekuwa wakipitia magumu sana. Ni wakati ambapo wameathiriwa na ugonjwa wa corona. Bila serikali kuwajali, ikaenda mbele kuongeza bei ya mafuta. Mhe. Spika, bei hii ambayo imeenda juu kwa wakati huu imeathiri pia bei ya chakula ambacho wananchi walikuwa wanataabika kutafuta pesa ili waweze kuweka mezani. Kwa sasa kuna shida nyingi kupata chakula kwa sababu mafuta ndiyo hutumika saa zingine kusaga au kutengeneza chakula na vilevile pia kukipeleka sokoni au pia wakati watu wanaenda sokoni kununua bidhaa hizi na wakati bidhaa zinapokuwa processed . Kwa hivyo ni jukumu letu sisi viongozi ambao tunawaongoza wananchi tuweze kuhimiza bei hii iweze kuenda chini na ushuru upunguzwe ili wananchi waweze kuyakidhi mahitaji yao. Hii ni kwa sababu wakati wa curfew haujaondolewa na wakati huo wananchi huwa wanasumbuka sana kujaribu kutafuta hela lakini kwa sasa hakuna muda wa kutosha wa kutafuta hela. Kwa hivyo ni lazima tuungane hapa tuweze kushughulikia jambo hili ili mwananchi aweze kusaidika. Vilevile, nashukuru sana kwa zile siku ambazo umepeana. Siku 14 sio nyingi sana. Jambo hili litaweza kushughulikiwa kwa haraka. Asante sana."
}