GET /api/v0.1/hansard/entries/110291/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 110291,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/110291/?format=api",
    "text_counter": 625,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Ms. Shakila",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 380,
        "legal_name": "Shakila Abdalla",
        "slug": "shakila-abdalla"
    },
    "content": "Asante, Bw. Naibu Spika. Nakushukuru kwa kunipa nafasi hii. Hakika, Katiba hii imechangiwa na watu wengi sana na hivi sasa, imefikia wakati wa kuchangiwa na Wabunge. Nawaomba wananchi wawapatie nafasi Wabunge wachangie Katiba hii na watoe maoni yao. Marekebisho ya Katiba ni lazima, na hakuna pahali pengine marekebisho haya yatafanyika isipokuwa katika Bunge hili. Ikiwa Bunge litafanya makosa na kupitisha Katiba hii bila ya marekebisho, itakuwa ni masikitiko makubwa. Kitu kingine, Bw. Naibu Spika, kwa sababu ya wakati, nataka nigusie juu ya Kadhis’ Courts. Mkenya yeyote, kabila au dini yoyote inahukumiwa na korti ya Kenya. Sababu ya hii korti kuitwa Kadhis’ Court ni kwa sababu inasimamia mambo mawili ambayo Korti ya Kenya haiwezi kuhukumu kulingana na dini. Kwa hivyo, ikiwa kuna dini yoyote ambayo ina pingamizi kuhusu Waislamu--- Shughuli za kuoana, kuachana na urithi wa Waislamu ni lazima zisimamiwe na Kadhi. Kama kuna watu walio na pingamizi kuhusu jambo hili, wana uhuru wa kuleta malalamishi yao na marekebisho yafanywe katika Katiba. Lakini kusema kwamba Kadhis’ Courts zitolewe itakuwa sio haki, na ni kama kuwanyima baadhi ya Wakenya haki zao za kibinadamu. Bw. Naibu Spika, upande wa abortion ---"
}