GET /api/v0.1/hansard/entries/1103024/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1103024,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1103024/?format=api",
    "text_counter": 67,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "Asante, Bw. Spika. Kwanza ningependa kumpa kongole dada yetu, Sen. Kwamboka, kwa kuleta hii Taarifa. Kulingana na vile sisi na wananchi wanaona, Mheshimiwa Rais aliweka mkazo ili watu wawe wameenda nyumbani ikifika Saa Tatu. Lakini, tunaona kuwa kuna shida ya kutekeleza agizo hili kwa sababu kwa upande mwingine, wafanyabiashara wa aina mbali mbali wanafunga maduka yao Saa Mbili ili waweze kwenda nyumbani Saa Tatu na wafike kwa nyumbani Saa Nne. Wafanyabiashara wamepata taabu kwa upande wa ubaguzi. Ukiangalia upande wa Nairobi West, utaona kwamba watu wanalazimishwa kufunga biashara zao, na kwingine, watu wanaruhusiwa kuendelea. Hii yote inaletwa kwa sababu ya kuzembea kwa kutengeneza sheria kwamba ikifika Saa Tatu, kila mtu anatakiwa kufunga biashara yake. Kuzembea huku hauko Nairobi pekee, bali katika sehemu za Pwani pia. Upande wa Kilifi kuna maeneo mengine ambayo yanaruhusiwa baa kuendesha shughuli zao mpaka Saa Tatu. Ni wazi kabisa mbele ya polisi wakiona, ilhali kuna biashara zingine zinasimamishwa mapema sana. Maduka ambayo watu wanaweza kununua vitu yanafungwa mapema ili watu waende nyumbani kutekeleza wajibu wa kuzuia watu wasitoke usiku. Inafahamika wazi kabisa kuwa kuna watu wengine wanaruhusiwa kuendelea kufanya biashara zao. Kwa hivyo, sheria ya COVID-19 inayofanya watu wazuiliwe na wanaambiwa kuwa Saa Tatu wawe wameenda iwe inafanywa kwa usawa. Ikiwa ni Saa Tatu, biashara zote zifungwe Saa Tatu. Sio eti wengine wanafunga Saa Moja na wengine wanafunga Saa Tatu. Asante, Bw. Spika."
}