GET /api/v0.1/hansard/entries/1103030/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1103030,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1103030/?format=api",
    "text_counter": 73,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Asante, Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii kuunga mkono Taarifa iliyoletwa Bungeni na Sen. Kwamboka. Hivi majuzi, mahakama ilitangaza kuwa kanuni za curfew ni haramu na hazifai kutekelezwa. Amri hiyo ilitolewa na High Court hapa Nairobi, na kuendelea kutumika kwa kanuni za curfew ni kinyume cha sheria na amri ya mahakama. Jambo la pili ni kuwa kanuni za curfew zinazotangazwa mara kwa mara ni lazima ziletwe Bungeni ili ziangaliwe, zichunguzwe, na kupitishwa kama inavyosema StatutoryInstruments Act (2013). Kutoka mwaka jana tulipomaliza na kamati maalum ya COVID- 19, mpaka sasa sijaona regulations zozote ambazo zimeletwa hapa Bungeni zinahusiana na mambo na curfew au jambo lolote linalohusika na mwelekeo wa mambo ya COVID- 19 katika nchi ya Kenya. Kama Mwenyekiti wa Kamati ya Delegated Legislation, hatujaletewa kanuni zozote. Kwa hivyo, kanuni zinazotumika kwa sasa ziko kinyume cha sheria na haifai Bunge kunyamazia jambo kama hili. Asante, Bw. Spika."
}