GET /api/v0.1/hansard/entries/1103050/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1103050,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1103050/?format=api",
"text_counter": 93,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Mhe. Bw. Spika, nasimama kwa hoja ya nidhamu. Sen. Olekina ni rafiki yangu sana, lakini ikifika kuendesha ratiba ya Bunge sawasawa tunatengana. Amesema kwamba yeye kama mmoja wa wale viongozi katika taifa hili kuna mahali wanapokwenda kustarehe mpaka saa kumi alfajiri na polisi wanapajua. Hatutaki kujuwa wanajivinjari na nani? Wanajivinjari mpaka saa hizo na wale ambao hawajiwezi, kwa mfano, wanaojivinjari pale Nairobi West, wanaambiwa wafunge hizo baa au sehemu za kustarehe saa moja jioni. Kama alivyosema wao hustarehe hadi saa nane ya usiku. Ukisema jambo kama hilo Bungeni ni lazima utaje mahali hapo. Je, ni haki kwake kuongea bila kutaja mahali hapo? Je, anaweza kueleza Bunge hili ni watu gani hao wanaoketi mpaka saa tisa alfajiri na polisi wanaogopa kwenda kuwashika?"
}