GET /api/v0.1/hansard/entries/110306/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 110306,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/110306/?format=api",
    "text_counter": 640,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Mung’aro",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 76,
        "legal_name": "Gideon Mung'aro Maitha",
        "slug": "gideon-maitha"
    },
    "content": "Nashukuru, Bw. Naibu Spika. Mimi pia nataka kuchangia nikisema kwamba Bunge hili lina jukumu la kuwapatia Wakenya Katiba mpya, lakini sio jukumu la kuwapatia Wakenya Katiba yoyote. Nataka kuunga mkono wenzangu walioongea na kusema kwamba tunahitaji Serikali--- Mimi sitasema kuhusu Serikali ya Mikoa kwa vile hakuna haja ya kuogopa tunaposema tunataka Serikali za Majimbo; Marekani, Ujerumani, India na nchi nyingine ambazo zimeendelea wamekuwa na serikali za Majimbo. Tunataka utawala uwe mashinani ili wananchi waweze kuchangia katika uongozi wa taifa hili. Tumeona kwamba utoaji wa huduma kwa wananchi wa nchi hii kila mara umefikwa na pingamiza kwa sababu ya Serikali kuu. Bw. Naibu Spika, nataka kusema jambo moja kuhusu swala la Ardhi, hasa katika Pwani. Ardhi imetumiwa miaka yote na wanasiasia kupeanwa kama zawadi ili wanaofaidika waunge mkono vyama vya wakuu Serikalini. Hilo ndilo jambo lililotuchosha na ndio maana tunataka Serikali za Majimbo. Asante, Bw. Naibu Spika. Naunga mkono."
}