GET /api/v0.1/hansard/entries/1103179/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1103179,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1103179/?format=api",
    "text_counter": 222,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "Jambo la pili ni kwamba hakuna hata siku moja ambapo Serikali ama nchi yetu imeshindwa kulipa madeni yake. Huwa tunafanya mipango ili madeni yote yalipwe. Sasa hivi kuna mabwenyenye wanaotumia akili. Kanuni za Hazina hiyo zinazotakikana kuwekwa na Benki Kuu ya Kenya ziko katika Hazina Kuu ya Taifa. Kuna watu katika Benki Kuu ya Kenya wanaotakikana kuhusika katika Hazina ya Kuzama. Wanafaa kuchangia na kuona kwamba sheria mwafaka zinafuatwa. Jambo la kusikitisha ni kwamba hawahusiswi katika kuangalia mambo ambayo yanaendelea katika Ofisi ya Fedha. Sababu ya mwisho ni kwamba usimamizi unaotakina kuangalia matumizi ya pesa sharti ufanywe kwa kuhusisha taasisi mbili. Kuna Benki Kuu ya Kenya na Hazina ya Taifa. Kulingana na sheria, ikiwa taasisi moja haihusiswi katika kamati inayoangalia jinsi pesa zinavyotumiwa, basi kutakuwa na shida kubwa kwa sababu hao ndio wanaoweza kuangalia matumizi ya pesa ama jinsi madeni yanavyolipwa."
}