GET /api/v0.1/hansard/entries/1103602/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1103602,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1103602/?format=api",
"text_counter": 68,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Asante Bw. Spika kwa kunipa fursa hii. Kwanza, ninampongeza Sen. Omanga kwa kuleta Taarifa hii katika Bunge la Seneti. Yeye ni msimamizi wa wanyonge katika nchi yetu ya Kenya. Swala la polisi kutoajibika limezungumziwa kwa muda mrefu hapa katika Bunge la Seneti. Wiki iliyopita, tulizungumzia swala la kupoteza Prof. Abdisalam na mfanya biashara Abdulahakim Sagar kule Mombasa. Maajabu ni kuwa watu hao wawili waliachiliwa huru usiku wa Jumapili na Jumamosi katika maeneo ambayo ni mbali na manyumba yao na hatari kwa usalama."
}