GET /api/v0.1/hansard/entries/1103613/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1103613,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1103613/?format=api",
"text_counter": 79,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Bw. Spika, utenda kazi wa polisi umekuwa ukimulikwa mara mara na Bunge la Seneti. Hadi hatua muhimu zichukuliwe dhidi ya polisi, hakuna jambo lolote litafanyika kwa sababu, kila wiki, visa vya kutowajibika kwa polisi vinaongezeka. Mwezi ulioisha ilikuwa ni Mombasa, juzi ikawa Nairobi na tena Nairobi, na mwezi huo mwingine ilikuwa Laikipia. Visa bado vinaendelea kutokea. Kwa hivyo, ninaomba swala hili lijadiliwe sio na Kamati ya Usalama pekee yake lakini pia Kamati ya Sheria na Haki za Binadamu. Yale yanayotendeka sio kinyume cha usalama pekee, ni kinyume cha Katiba yetu. Kwa hivyo, Kamati husika inafaa ichunguze swala hili. Hapo awali nilipokuwa kwenye Kamati hii, tulizunguka katika sehemu tofauti tofauti kuchunguza maswala ya kuuliwa kiholela kwa raia wa nchi ya Kenya. Hadi leo, ripoti hiyo haiijaletwa Bungeni. Kwa hivyo, nina omba uamrishe Kamati ya Sheria ilete ripoti ili tuijadili na kutoa mwongozo vipi sheria itatekelezwa."
}