GET /api/v0.1/hansard/entries/1103641/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1103641,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1103641/?format=api",
    "text_counter": 107,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Katiba yetu inalinda haki ya mwananchi kutetea haki yake kwa njia ya maandamano, kama vile wanabiashara waliokuwa na Bw. Alex Macharia walifanya kutetea haki yao. Bi. Spika wa Muda, kubomoa biashara na manyumba za watu ni njia duni nchi kama yetu iliyo na demokrasia inaweza kutumia askari wake kuumiza wanachi wake. Ingewezekana, tungepata Kamati inayo ongozwa na Sen. Outa. Angechukua hatua kali sana kuhakikisha kwamba mkuu wa polisi na Waziri wa Interior and Coordination of National Government wana wajibika. Tusikuje hapa kusoma Taarifa hii kwa Bunge na kuonekana na wananchi na hakuna haki ina tendeka. Tunataka tuone kwamba polisi wetu wanawajibika kwa njia ambayo wanafanya kazi yao na wanalinda maisha ya mwananchi wa kawaida. Bi. Spika wa Muda, nashukuru Sen. Omanga kwa kuchukua nafasi hii kutetea Bw. Macharia, familia yake, na wale wote ambao wamekandamizwa kwa polisi kutumia nguvu. Asante, Bi. Spika wa Muda."
}