GET /api/v0.1/hansard/entries/1103667/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1103667,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1103667/?format=api",
"text_counter": 133,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Murkomen",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 440,
"legal_name": "Onesimus Kipchumba Murkomen",
"slug": "kipchumba-murkomen"
},
"content": "Bi. Spika wa Muda, swali hili lililoletwa na Sen. Sakaja ambaye ni Seneta wa Kaunti ya Jiji la Nairobi ni la maana sana. Kwanza kabisa hali ya afya katika kaunti zetu, si Nairobi tu, iko na shida kubwa sana. Sijui hali ya Kisumu Kaunti unapotoka, Bi. Spika wa Muda, lakini Elgeyo Marakwet ninakotoka, kazi iliyofanywa na serikali za kaunti katika muhula wa kwanza wa ugatuzi ilikuwa bora kuliko wale wamefanya katika muhula wa pili hasa magavana wanaomaliza muhula wao wa pili. Nilikuwa Elgeyo Marakwet mwishoni mwa juma. Hospitali kuu ya Iten iko katika hali hatari sana. Wagonjwa wengi wanalala sakafuni na kukusanywa pamoja, walio na COVID-19 na wasio. Hali ni vivyo hivyo katika kaunti ya Kitui. Sen. Wambua alituonyesha na pia kupitia vyombo vya habari kwamba hata mbuzi wanaishi katika hospitali za Kitui. Wagonjwa wamerundikwa katika chumba kimoja. Nilishangaa juzi kuwa Gavana wa Kitui amenunua malori ya kusafirisha mbuzi lakini hana magari ya kupeleka wagonjwa hospitali. Bi. Spika wa Muda, unajua ni kwa nini kaunti nyingi haziweki pesa nyingi kwa mambo ya afya na hospitai? Ni kwa sababu zile dawa hazileti kandarasi za kuwawezesha"
}