GET /api/v0.1/hansard/entries/1103681/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1103681,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1103681/?format=api",
    "text_counter": 147,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Sakaja",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13131,
        "legal_name": "Johnson Arthur Sakaja",
        "slug": "johnson-arthur-sakaja"
    },
    "content": "Bi. Spika wa Muda, nina hoja ya nidhamu. Ingawa nakubaliana na mambo kadha wa kadha aliyonena Sen. Murkomen, singependa ampotoshe Maj. Gen. Badi kuwa hafai kualikwa na kufika mbele ya kamati za Seneti. Maj Gen. Badi lazima awajibike. Katiba inaruhusu Seneti kualika mtu yeyote ili kuangazia mambo yanayo athiri wananchi. Maj. Gen. Badi alijiwasilisha mbele ya Kamati ya Afya ya Senenti mapema leo. Maj. Gen. Badi anapaswa kufahamu kuwa lazima awajibike na kujibu maswali ya viongozi walichaguliwa kuwakilisha wananchi. Tulimpa Maj. Gen. Badi kazi na kwa hivyo hana budi ila kuwajibika na kujibu maswali kuhusu yote yanayo waathiri wakaazi wa Kaunti ya Nairobi. Naomba Sen. Murkomen kutompotosha Maj. Gen. Badi kufikiria kwamba hafai kuwajibika. Lazima mkuu wa NMS aje mbele ya kamati yoyote ya Seneti itakayo mualika kuangazia jambo lolote. Nimeona Kaunti ya Nairobi inakumbwa na changa moto kadha wa kadha. Hivyo nimeamua kuwania kiti cha gavana wa Kaunti ya Nairobi mwaka ujao kama raia wa kawaida. Mimi sio mwanajeshi hivyo nina imani kuwa nitaendelesha kazi vizuri."
}