GET /api/v0.1/hansard/entries/1103683/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1103683,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1103683/?format=api",
    "text_counter": 149,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "September 23, 2021 SENATE DEBATES 14 Sen. Murkomen",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Bi. Spika wa muda, nakubaliana na Sen. Sakaja kuwa kisheria, hakuna yeyote ambaye hawezi kualikwa mbele ya kamati yoyote ya Senenti kuwajibika. Kwa hivyo ni lazima Maj. Gen. Badi afike mbele ya kamati yoyote ya Bunge itakayo mualika kujibu maswali. Hata hivyo, ni jana tu tulikuwa tunajadili hoja ya kuwashutumu Mhe. John K. Munyes, Waziri wa Petroli Na Uchimbaji Madini na Mhe. Charles Keter, Waziri Wa Kawi, ambao walikosa kutambua mwaliko na kuja mbele ya kamati za Seneti. Kama mawaziri, ambao ni wananchi wa kawaida, hawatambui mwaliko wa Seneti, je Maj. Generali, ambaye ni mwanajeshi, atambua mwaliko kweli? Ni kwa sababu ya changamoto kama hizo zinazokumba Kaunti ya Nairobi zinafaa kutatuliwa mara moja. I wish Maj. Gen. Badi was a retired general."
}