GET /api/v0.1/hansard/entries/1104461/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1104461,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1104461/?format=api",
"text_counter": 211,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kuria East, JP",
"speaker_title": "Hon. Marwa Kitayama",
"speaker": {
"id": 13394,
"legal_name": "Marwa Kemero Maisori Kitayama",
"slug": "marwa-kemero-maisori-kitayama"
},
"content": " Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Naomba nianze kwa kumshukuru mwenzangu, Mhe. (Dkt.) Pukose, kwa Mswada huu. Ninaunga mkono ila kwa marekebisho. Ni vizuri kwamba Mswada huu umeonyesha, kuanzia mwanzo, kwamba unataka kuboresha maisha ya Wakenya kwa upande wa madawa, lishe na afya zetu. Nimefurahishwa sana na Mswada huu kwa sababu unalenga kuhakikisha kuwa madawa ambayo tunapata kama wananchi wa Kenya ni kulingana na maagizo ya daktari ili ukinunua dawa ni nzuri kwa afya yako. Hiyo ndiyo sababu ninasema kuwa tunahitaji kuwa na marekebisho tusije tukawa na Mswada ambao badala ya kurahisisha kufikia huduma ya afya, unapinga mtu ambaye anatoka sehemu pembezoni - mfano yule mama ambaye anaishi mahali panaitwa Biasimui ama Ngochoni - asiweze kufikia na kununua dawa kwa sababu hakupata daktari ambaye ataandika dawa ile anayohitaji kutumia. Kwa hivyo, kuna haja ya sisi kukubali kwamba Mswada huu The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}